Connect with us

Makala

Messi Atwaa Ballon D’or

Mshambuliaji Lionel Messi amefanikiwa kutwaa tuzo yake ya nane ya mchezaji bora wa kiume duniani kwa mwaka 2023 akiwashinda Kylian Mbappe na Eerlin Haaland ambao aliingia nao fainali katika tuzo hizo maarufu duniani.

Ballon D’or ambayo mshindi hupatikana kwa kupigiwa kura na makocha wa timu za taifa pamoja na manahodha na baadhi ya waandishi wa habari za michezo wateule hufanyika kila mwaka ikiwa chini ya usimamizi wa jarida maarufu nchini Ufaransa (French Magazine).

Messi mwenye umri wa miaka 36 ametwaa tuzo hiyo ya nane kwake baada ya kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutwaa tuzo ya kombe la dunia mwaka jana huku staa wa uingereza Judde Bellingam ameshida tuzo ya Kopa ya mchezaji bora chini ya miaka 21.

“Ni vizuri kuwa hapa na zaidi kufurahi muda huu adhimu kabisa kushinda kombe la dunia na kufurahia kutimiza ndoto zangua”Alisema Messi

Erlin Haaland yeye ameshinda tuzo ya Gerd Muller ya kufunga mabao mengi zaidi ambapo aliweka rekodi ya kufunga mabao 36 katika michezo 35 ya ligi na kufikisha mabao 52 katika michuano yote huku akishinda makombe matatu ya ligi kuu ya Uingereza,Kombe la klabu bingwa barani ulaya na kombe la shirikisho.

“Nataka niishukuru Manchester City na klabu nzima kwa ujumla pia ninaishukuru familia yangu na watu wote wanaonizunguka wanaonifanya niwe hapa nilipo leo”Alisema Haaland

Katika tuzo hizo kipa wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Aston Villa Emiliano Martinez alishinda tuzo ya Yashin ya kipa bora akiiwezesha Argentina kushinda fainali ya kombe la dunia baada ya kuokoa penati ya Kingsley Coman huku pia akiiwezesha klabu yake ya Aston Villa kumaliza katika nafasi ya saba ya ligi kuu na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Uefa Conference  League.

Klabu ya Manchester City yenyewe imefanikiwa kuchukua tuzo ya klabu ya mwaka baada ya kufanikiwa kutwaa mataji matatu ya ligi,klabu bingwa ulaya na kombe la shirikisho huku ikitoa wachezaji saba katika orodha ya wagombea wa tuzo ya wachezaji bora wa dunia.

Katika usiku huo mchezaji wa klabu ya Real Madrid Vinicius Jr amepokea tuzo ya Socrates kwa juhudi zake za kupinga ubaguzi wa rangi nje na ndani ya uwanja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala