Connect with us

Makala

Messi Atambulishwa Marekani

Klabu ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu ya soka Marekani (MLS) usiku wa kuamkia leo Jumatatu wamewatambulisha rasmi nyota wa Argentina Lionel Messi mbele ya washabiki zaidi ya 19,000 kwenye uwanja wao wa nyumbani DRV PNK Stadium.

Messi amejiunga na Inter Miami katika majira haya ya kiangazi baada ya mkataba wake na PSG kumalizika huku pia mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Sergio Busquets nae ametambulishwa kwenye timu hiyo ambapo amepewa jezi namba 5.

Messi aliamua kuondoka nchini Ufaransa katika klabu ya Paris St.German ambapo alijiunga akitokea klabu iliyomkuza ya Fc Barcelona licha ya kuwa na tetesi za kujiunga na timu za Uarabuni lakini mwishoni alijiunga na InterMiami inayoshiriki ligi kuu ya Major League Soccer ambayo hufupishwa kama Mls.

Katika utambulisho pia matajiri wanaomiliki klabu hiyo walikuwapo wakiongozwa na David Beckham ambaye ana hisa klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala