Connect with us

Makala

Mchonganishi Simba ,Yanga Anukia Morocco

Kiungo wa Polisi Tanzania,Baraka Majogoro anayewindwa na Simba, Yanga na Azam FC huenda akasepa zake na kuibukia Morocco kukipiga kwenye soka la kulipwa kwani kuna timu moja imeingia kwenye 18 za kuisaka saini ya nyota huyo.

Majogoro msimu huu amekuwa kwenye ubora wake hata amekuwa akizichonganisha Simba na Yanga ambazo zote zinahaha kuipata saini yake.

Kiungo huyo anachotazama zaidi ni nafasi yake ya kucheza kwanza na tayari  ameanza mazungumzo na klabu ya Youssofia Berrechid ya huko Morocco hivyo mambo yakijibu anaweza kusepa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala