Connect with us

Makala

Mbrazil Atua Singida FG

Klabu ya Singida Big Stars imemtambulisha rasmi kocha wao mpya Ricardo Ferreira kutoka nchini Brazil ambaye anakuja kuchukua nafasi ya kocha Enrst Middendorp ambaye aliamua kujiuzuru ghafla kuifundisha timu hiyo.

Kocha Ricardo ana rekodi ya kufundisha vilabu vikubwa barani Afrika kwa mafanikio vikiwemo Al Hilal, Al Merrikh SC na Ismaily SC hivyo anatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwa klabu zinazokutana na timu hiyo hasa katika ligi kuu nchini.

Kocha huyo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuinoa timu hiyo ambapo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mathias Lule na Thabo Senong waliokuwa wanaiongoza baada ya kuondoka kwa kocha mkuu Ernst Middendorp.

Tayari timu hiyo iliamuajiri kocha Peter Manyika kuja kuwanoa makipa wa klabu hiyo huku ikitajwa kuwa kocha Zubeiry Katwila pia anakuja kuungana nae kama kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala