Connect with us

Makala

Mbaraka Arudi Nyumbani Kagera Sugar

Mchezaji wa Azam Fc,Mbaraka Yusuph amesaini kandarasi ya miaka miwili kuichezea timu yake ya zamani ya Kagera Sugar baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya Azam.

Mbaraka alisajiliwa hapo awali na Azam Fc akitokea Kagera Sugar baada ya kuwa mfungaji bora ila kwa sasa anarejea nyumbani Bukoba kutokana na kutokuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi hicho kwa takribani miaka mitatu huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Baada ya kusaini mkataba huo Mbaraka amesema kuwa ni wakati wake wa kurejea nyumbani na yupo tayari kuucheza mpira haswa kwani ni mchezaji huru kwa sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala