Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Kalala Mayele amezidi kuonyesha ubora wake kiwanjani huku akifunga mabao ya kideoni katika michezo ya ligi kuu nchini hasa bao la siku ya Jumanne alilowafunga Mtibwa Sugar katika ushindi wa mabao 3-0 uliopata klabu yake ya Yanga sc dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na kufikisha alama 10 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.
Mayele alifunga bao la pili kwa Yanga sc baada ya Djuma Shabani kufunga bao la kwanza kwa faulo ambapo pasi ya Dickson Job ilimkuta Salum Abubakari ambaye alimpasia Farid Musa ambaye akampasia Mayele pasi ya mpenyezo iliyowashinda mabeki ya Mtibwa Sugar na kumkuta Mayele ambaye aliwapiga chenga mabeki wa kati wawili kisha akampiga tena chenga beki mwingine na kumkuta kipa Farouk Shikalo na kufunga bao hilo kali.
Licha ya bao hilo tayari Mayele alikua ametoka kufunga bao jingine kali dhidi ya Zalan Fc akifunga kwa kisigino akiunganisha shuti la Feisal Salum na pia akikumbukwa kwa kufunga bao la Tiktak msimu uliopita dhidi ya Kagera Sugar ambapo mabao yaote haya yamefananishwa na yale ya nguli wa soka Diego Maradona ambaye alifunga mabao makali akiwatoka mabeki kwa spidi na chenga kali.
Mpaka sasa Mayele ana mabao matatu ya ligi kuu huku akiwa amefunga mabao matatu pia katika michuano ya kimataifa aliyofunga dhidi ya Zalan Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa katika hatua ya awali uliofanyika katika uwanja wa Mkapa siku ya Jumamosi iliyopita.