Connect with us

Makala

Maxi Nzengeli Aimaliza Singida FG

Mabao mawili ya Maxi Mpia Nzengeli yametosha kabisa kuimaliza Singida Fountain Gate Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya klabu ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ikianza na mabadiliko ya wachezaji wawili Hafidh Nkokoni na Zawadi Mauya kutoka katika kikosi chake cha kila siku Yanga sc ilifanikiwa kutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku uwezo wa mabeki Yao Yao na Joyce Lomaliza upande wa pembeni ukiwabeba zaidi.

Singida FG iliteseka na pengo la kumkosa kipa wake Benno Kakolanya na beki Hamad Waziri kwani iliruhusu mashambulizi mengi huku kipa Benedict Haule akishindwa kuicheza krosi ya Yao Yao ambayo ilizaa bao la kwanza kutoka kwa Maxi kwa kichwa dakika ya 30 ya mchezo.

Dakika tisa baadae Nzengeli alifumua shuti kali lililomshinda kipa Haule na kuiandikia Yanga sc bao la pili la mchezo huo ambalo lilidumu mpaka mapumziko ya kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili licha ya mabadiliko kutoka pande zote katika dakika 45 wakiingia Mahalatse Makudubela Skude,Salum Abubakar,Clement Mzize,Kennedy Musonda,Nickson Kibabage kwa upande wa Yanga sc huku upande wa Singida wakiingia Deus Kaseke,Morice Chukwu,Meddie Kagere ambapo pamoja na mabadiliko hayo bado dakika 90 zilimalizika kwa Yanga sc kuondoka na alama zote tatu.

Yanga sc sasa imejichimbia kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 18 huku Simba sc ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 15 ikiwa na michezo miwili mkononi na Singida Fountain Gate yenyewe imesalia katika nafasi ya saba ikiwa na alama nane.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala