Connect with us

Makala

Mastaa Tisa Yanga sc Kuikosa Biashara

Wakati kikosi cha Yanga sc kikitarajiwa kuingia uwanjani muda mfupi ujao imebainika mastaa tisa wataukosa mchezo huo wa hatua ya 16 ya kombe la shirikisho la Azam Sports utaofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Orodha ya mastaa hao Djuma Shabani na Dickson Job ambao wanatumikia adhabu ya kufungiwa huku Djuma akitarajiwa kuwepo mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar na Job ndo anaanza adhabu ya mechi tatu kwa kumkanyaga Richarlson Ng’ondya wa Mbeya City wakati walipokutana katika mchezo wa ligi kuu.

Mastaa kama Chico Ushindi,Yassin Mustapha,David Bryson,Kibwana Shomari,Abdala Shaibu,Salum Abubakary,Chrispin Ngushi wenyewe wanasumbuliwa na majeraha mbalimbali huku Yacouba Sogne akiwa amerejea tayari baada ya kuwa nje kwa miezi mitatu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala