Connect with us

Makala

Masoud Djuma Kocha Mpya Dodoma Jiji

Klabu ya soka ya Dodoma jiji Fc yenye makao yake makuu jijini Dodoma imemuajiri kocha wa zamani wa klabu ya Simba sc Masoud Djuma kama kocha mkuu waklabu hiyo kufuatia kuachana na kocha Mbwana Makata.

Djuma anachukua nafasi hiyo baada ya Makata kutimuliwa klabuni hapo kutokana na matokeo mabovu ambapo timu hiyo Ndani ya michezo mitano iliyopita, Makata alijikuta akiongoza Dodoma Jiji kuambulia pointi moja tu dhidi ya Geita Gold na kukumbana na vipigo vinne, ikiwemo vitatu mfululizo ambavyo ni kama vilikoleza kuota nyasi kwa kibarua chake makao makuu ya nchi.

Makata ambaye Mchezo wa mwisho kukaa kwenye benchi ilikuwa ni Februari 20 uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na ubao ulisoma KMC 2-0 Dodoma Jiji nafasi yake inachukuliwa na kocha huyo ambaye ametambulishwa rasmi klabuni hapo akiwa na kazi ya kupandisha kiwango cha timu hiyo katika duru la pili la ligi kuu nchini.

Dodoma jiji hivi sasa ipo katika nafasi ya 11 ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 17 katika michezo 15 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala