Msemaji wa Ruvu Shooting Masu Bwire ameonekana akiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya kujiandaa kuanza kwa kilele cha tamasha la Simba day katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Mwalim huyo wa somo la hisabati mwenye mbwembwe kipau anapokua akiisemea Ruvu Shooting ama kuongelea mpira alianza kuzua maswali alipoonekana akiwa amevaa barakoa ya Simba katika hafla ya kuaga mwili wa Hanspoppe viwanja vya Krimjee hivi karibuni.
Masau ameonekana tena leo katika dimba la Mkapa akionekana kuwa na mafundi mitambo wakikagua baadhi ya mitambo uwanjani hapo akionekana pia kushika kipaza sauti,hali inayoonesha kuwa huenda akasheherehesha tamasha hilo.
Kaimu Afisa hbari wa Simba Ezekiel Kamwaga anatarajia kumaliza muda wake hivi karibuni na huenda Masau akachukua nafasi hiyo.endapo Masau akipata nafasi hiyo itanogesha zaidi utamu wa utani wa jadi wa Simba na Yanga ukizingatia uwepo wa Haji Manara Yanga SC.
Leo ni kilele cha tamasha kubwa la Simba day ambapo shamrashamra zinaendelea katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo kutokuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mashabiki wa Simba,mechi za timu za vijana na timu ya wanawake ya Simba Queens,utambulisho wa wachezaji wapya na wale wa zamani,benchi la ufundi,kabla ya kuhutimishwa kwa mtanange mkali kati ya Simba na mabingwa wa DR Congo TP Mazembe .
Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo anatarajiwa kuwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai.