Connect with us

Makala

Manula Arejea Rasmi

Sasa ni rasmi klabu ya Simba sc imetangaza kurejea kwa kipa Aishi Manula aliyekua na majeraha ya muda mrefu ambapo alikaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi takribani sita sasa baada ya kuumia goti na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Simba sc ni rasmi kipa huyo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kumaliza programu maalumu ya kurejeza utimamu wa mwili aliyokua anafanya pekee yake ili arejee katika hali yake ya kawaida.

Kuumia kwa Manula ilikua pengo kubwa kwa klabu hiyo hasa baada ya kuondoka kwa kipa Beno Kakolanya na hivyo kulazimika klabu hiyo kumtumia Ally Salim hali iliyozua hofu kwa mashabiki licha ya kipa huyo kujitahidi kuonyesha ubora mara kadhaa japo alikua na makosa machache.

Msimu huu klabu hiyo iliwasajili Hussein Abel na Ayoub Lakred ikiwa kama njia ya kukabiliana na pengo la Manula lakini mpaka sasa bado eneo hilo halijapata tiba sahihi kutokana na kiwango duni kinachooneshwa na Ayoub Lakred ambapo pia wakati mwingine huchangiwa na makosa ya timu kwa ujumla.

Manula amefanikiwa kudumu katika kiwango chake kwa muda mrefu tangu klabu hiyo imsajili kutoka Azam Fc pamoja na Erasto Nyoni,John Bocco na Shomari Kapombe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala