Connect with us

Makala

Mangungu Atetea Kiti Simba sc

Mwenyekiti wa klabu ya Simba sc Murtaza Mangungu amefanikiwa kutetea nafasi hiyo katika klabu ya Simba sc baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwl.Julius Nyerere uliopo Posta jijini Dar es salaam.

Mangungu alikua anawania nafasi hiyo pamoja na wakili Moses Stewart Kaluwa ambaye katika uchaguzi huo alipata kura 1045 huku Mangungu akishinda kwa jumla ya kura 1311 na kufanikiwa kurejea katika nafasi hiyo aliyoikalia baada ya Swedi Nkwambi kujiuzuru.

Mbali na nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo pia kulikua na nafasi za wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ambazo zilikua zinagombewa ambapo jumla ya wanachama 2363 walipiga kura na washindi ni kama ifuatavyo.

▪️Dkt. Seif Ramadhani Muba [Kura 1636]
▪️Asha Baraka [Kura 1,564]
▪️CPA Issa Masoud Iddi [Kura 1,285]
▪️Rodney Makamba Chiduo [Kura 1,267]
▪️Seleman Harubu Said [Kura 1,250]

Wajumbe hao wataungana pamoja na Mwenyekiti pamoja na Afisa mtendaji mkuu wa klabu pamoja na wajumbe upande wa mwekezaji katika kufanya maamuzi mbalimbali kwa faida ya klabu ya Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala