Connect with us

Makala

Mane Anasepa! Liverpool Mtaelewa?

Mashabiki wa Liverpool wanaomba leo,kesho janga la corona liishe ili wamalize kazi yao ya kulisaka taji la kwanza la ligi kuu England (EPL) tangu walipolitwaa 1990,ila kwa sasa wajiandae tu kupata mshtuko kwani nyota wao Sadio Mane ameonekana kwenye anga za Real Madrid.

Kwa upande wa Los Blancos wamedaiwa kutenga kiasi cha pauni milioni 132 ili kumng’oa fowadi huyo wa kimataifa wa Senegal na kukinukisha Santiago Bernabeu.

Mane amekuwa na mguu mzuri tangu atue Liverpool mwaka 2016 akitokea Southampton na kwa msimu huu pekee amefunga mabao 14 na kutoa asisti 7,huku msimu uliopita aliisaidia timu hiyo kutwaa ushindi wa ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na kiwango cha ubora wake kimewafanya Madrid kummezea mate hata kuweka pauni 132 milioni mezani ili kumnasa nyota huyo aliyeifikisha Senegal kwenye fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

Sadio amekuwa akiiota Madrid kwenda kukipiga na sababu ya mane kutimkia huko ni kutokana na kuchochewa zaidi na Msenegal mwenzake Keita Balde aliyefichua kuwa nyota huyo hataki kusalia Anfield aliyoichezea mechi 118 za ligi kuu na kuifungia mabao 59 hadi sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala