Connect with us

Makala

Manchester City Baba Lao

Timu za Uingereza Manchester City na Aston Villa zimecheza jana katika uwanja wa Villa Park kwa kusimamiwa na refa Jonathan Moss kutoka wa nchini humo.

Manchester City imeshinda kwa mabao 6-1 katika mchezo huo ambapo goli la kwanza lilifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 18 na dakika ya 24 mchezaji huyo kuongeza tena bao la pili.

Sergio Aguero alifunga bao la tatu dakika ya 28 na kabla ya kwenda kipindi cha mapumziko dakika ya 45 Gabriel Jesus aliongeza bao la nne .

Katika kipindi cha pili cha mchezo Sergio Aguero aliongeza bao la tano dakika ya 57 na la sita dakika ya 81 huku upande wa Aston Villa walifunga bao moja kutokana na penati aliyopewa Anwar El Ghazi dakika ya 90.

Manchester City kwa sasa imekuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 katika mchezo wake wa 22 wa ligi kuu na Aston Villa ikishika mkia nafasi ya 18 ikiwa na pointi 21.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala