Connect with us

Makala

Manara Arejesha Fedha Yanga

Msemaji wa klabu ya Simba sc Haji Sunday Manara amefika makao makuu ya klabu ya Yanga sc kurejesha kiasi cha pesa alichochangiwa na mashabiki wa timu hiyo wakati akiwa mgonjwa wa miaka kadhaa iliyopita.

Manara aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa macho alitakiwa kuhudhuria matibabu nchini India hivyo mashabiki wa Yanga wakiongozwa na aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo kipindi hicho Jerry Muro waliamua kuchanga kiasi cha fedha na kwenda kumkabidhi kama sapoti ya matibabu.

Manara amerejesha fedha hizo baada ya Jerry Muro ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Arumeru kumtania kuhusu kuchangiwa huko hali iliyomkasirisha Manara na kufanya kurudisha fedha hizo ambazo hata hivyo hakufanikiwa baada ya kutowakuta viongozi wa klabu ya Yanga katika makaa makuu.

Msemaji huyo ameandika katika mtandai wa instagramu kuhusu tukio hilo ambapo aliandika ifuatavyo.

Nilikwenda mwenyew mchana huu klabuni Yanga,bahati mbaya sana sikuwakuta viongozi wa klabu,,Wazee niliowakuta nje baada ya kuwaeleza nimekuja kukabidhi pesa za masimango walinisihi sana nisifanye hvyo na wakaniambia yule ni mgeni hapa mjini na hajui tamaduni zetu na kuniomba nisirejeshe hata thumni… Nimefundishwa kuwatii wazee, na ntarejea kwa Wanasimba walionikabidhi pesa zao,,,busara itawashauri tupeleke hospitali kwa wagonjwa wasiojiweza,,ikiwapendeza tutafanya hvyo!!
Kwetu nimefundishwa uungwana,,kwetu nimepata malezi bora,,kwetu wazazi wangu walinijaza na Jeuri ya kutokubali kuonewa wala kunyanyaswa… halaf mm sijatoka Mbwinde,,hilo ni Muhimu sana na ndio maana naweza kuwa Msemaji pekee naweza kwenda klabu nyingine tena mchana kweupeeeee..

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala