Connect with us

Makala

Simba Inajipigia Tu

Simba Sc imeendelea kuonyesha ubabe baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Azam fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Azam fc ndio walianza kuandika bao dakika ya 5 kupitia kwa Nevere Tegere na Simba walisawazisha dakika nne badae kupitia kwa Erasto Nyoni huku Dakika ya 14 Deo Kanda aliongeza msumari wa pili na kuifanya Azam FC kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja huku Simba ikiongoza.

Iliwachukua Azam dakika nne za kipindi cha pili kusawazisha bao hilo kupitia kwa Idd Seleman bao ambalo lilidumu mpaka dakika 72 pale Meddie Kagere alipoongeza bao la tatu na ushindi kwa Simba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala