Connect with us

Makala

Man Utd Yatupwa Nje Uefa

Klabu ya Manchester united imeondoshwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kufungwa bao 1-0 na Atletico Madrid ya nchini Hispania na kuondolewa katika michuano kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 hapo awali.

Kipigo hicho kinaifanya Man united kumaliza msimu huu bila taji lolote baada ya kuondolewa katika mashindano mengine ya kombe la Fa na kombe la Carabao huku ikiwa hatihati kuingia katika nne bora ya ligi kuu ya Epl nchini humo.

Kocha Mkuu wa Manchester United Ralf Rangnick amesema kuwa walishindwa kutumia vizuri nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza jambo ambalo liliwafanya wapoteze mchezo wao.

”Tulikuwa na kipindi cha kwanza kizuri lakini tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulizipata ikawa bahati mbaya kwetu tukapoteza mchezo,”Alisema kocha huyo ambaye mashabiki wa Manchester United walikua na matumaini makubwa kwamba atafanya vizuri.

Katika mchezo huo licha ya Man united kufungwa pia staa wake Cristiano Ronaldo hakupiga hata shuti lililolenga lango katika dakika zote tisini ikiwa ni mara yake ya tatu katika maisha yake ya soka duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala