Connect with us

Makala

Man Utd Kukomaa na Anthony

Klabu ya Manchester United ina mpango wa kumchukulia hatua za kinidhamu Antony Santos kufuatia mashtaka yanayomkabili ya unyanyasaji na kutishia kifo ambayo amefunguliwa hivi karibuni na aliyekuwa mpenzi wake Gabriela Cavallin.

Staa huyo hivi karibuni ameingia katika kashfa ya kumfanyia ukatili mpenzi wake huyo kipindi ambacho walikua na mahusiano ikiwemo kumdhuru kimwili na kumtishia kumuondolea uhai wake kiasi cha mwanadada huyo kuamua kushtaki kwa jeshi la polisi nchini Brazil.

Kutokana na hilo Anthony tayari ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil huku pia ikibainika kuwa klabu yake ya Man united inafuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kubaini ukweli ndipo wachukue hatua stahiki.

“Klabu ya Manchester United inatambua kwamba tuhumu dhidi ya Antony zinafanyiwa kazi na jeshi la polisi  hivyo kwa sasa klabu itakaa kimya na itatoa tamko pale tuhuma hizo zitakapothibitika na kama klabu tunalichukulia suala hili kwa umakini mkubwa ukizingatia madhara  ya tuhuma hizi”.Ilisomeka taarifa hiyo

Antony ambaye alisajiliwa na United msimu wa 2022 kwa dau la paundi milioni 86 amekua na kiwango cha kupanda na kushuka uwanjani na hivyo kwa sasa anapaswa kujipanga kisaikolojia kukabiliana na tuhumu hizi ambapo yeye mwenyewe amezikanusha tayari.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala