Connect with us

Makala

Man Utd Aibu Tupu

Ni aibu,ndio neno fupi unaweza kusema kutokana na klabu ya Manchester United kupokea kipogo cha mabao 4-0 kutoka kwa mahasimu wao Liverpool katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool.

Iliwachukua Liverpool dakika 5 tu kupata bao la kwanza likifungwa na Luiz Dias kutokana na safu ya ulinzi ya Man united kutokua na maelewano ya kutosha chini ya nahodha Harry Maguire huku Mo salah akifunga bao la pili dakika ya 22 ya mchezo ambapo mpaka mapumziko matokeo yalibaki kuwa hivyo.

Kipindi cha pili kilikua kigumu zaidi kwa Man United kwani waliruhusu mabao mengine mawili kupitia kwa Mo salah na Sadio Mane huku umiliki w mchezo ukiwa ni asilimia 78 kwa Liverpool na 22 kwa Manchester United huku Liverpool wakipiga mashuti 5 golini kwa United ambapo mashuti manne yalizaa mabao huku Man Utd ikipiga shuti moja pekee.

Kutokana na matokeo hayo Liverpool wanasalia kileleni wakiwa na alama 76 huku Man United wakiwa nafasi ya sita na alama 54 katika michezo 33 ya ligi kuu nchini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala