Connect with us

Makala

Malone Arithi Jezi ya Mkude

Beki wa klabu ya Simba sc Che Fondoh Malone amekabidhiwa rasmi jezi namba 20 ambayo ilikua inavaliwa na kiungo Jonas Mkude aliyejiunga na klabu ya Yanga sc baada ya kuachwa na klabu ya Simba sc.

Awali Simba sc ilikua na mpango wa kuistafisha kwa muda jezi hiyo kuenzi mchango wa mchezaji huyo aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 13 huku pia wakiwa na mpango wa kumuaga siku ya Simba day lakini sasa uamuzi umebadilishwa na jezi hiyo sasa itavaliwa na beki huyo raia wa Cameroon.

Taarifa iliyotolewa hapo awali na msemaji wa klabu hiyo Ahmed Ally kuwa jezi hiyo itastaafishwa kwa muda fulani kutoa heshima kwa mkongwe hiyo.

Beki huyo alionekana siku ya mchezo wa kirafiki nchini Uturuki katika kambi ya maandalizi ya klabu hiyo akiwa kaivaa katika mchezo wa kirafiki wa pili nchini humo dhidi ya Turan PFK.

Mpaka sasa klabu hiyo bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu mabadiliko hayo huku pia baadhi ya wadau wakijiuliza kulikoni?

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala