Connect with us

Makala

Makocha Wafurika Simba sc

Meneja habari wa klabu ya Simba sc Ahmed Ally amesema kuwa makocha wengi kutoka barani ulaya wamejitokeza kuomba kazi katika klabu hiyo ili kurithi mikoba iliyoachwa wazi na Zoran Maki ambaye alivunja mkataba wake wa mwaka mmoja na kujiunga na klabu ya El Ittihad inayoshiriki ligi kuu nchini Misri.

Tayari klabu hiyo imetangaza kutafuta kocha mpya na katika mchakato huo tayari baadhi ya makocha wenye wasifu mkubwa barani Ulaya wametuma maombi ya kuhitaji nafasi hiyo ya kuifundisha klabu hiyo iliyotwa ubingwa wa ligi kuu mara 18 tangu kuanzishwa kwake.

“Makocha wengi wameomba, wengi wao ni kutoka nchi za bara la Ulaya, makocha wetu wazawa hadi sasa hakuna aliyekuomba nafasi hiyo, kama klabu imepanga zoezi la kupata kocha mkuu likamilike mapema kwa kuwa timu iko kwenye mashindano.” alisema Ahmed na kuongeza.

“Tunatarajia mchakato huo ukamilike mapema na kuwa na kocha mkuu, ambaye ataendeleza pale Mgunda atakapokuwa amefikia kwa kuwa hivi sasa yeye ni kocha mkuu wa muda.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala