Connect with us

Makala

Luis Mchezaji Bora Fainali FA

Kiungo wa Simba Sc, Luis Miquissone leo Agosti 2,2020 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Luis amehusika kwenye mabao yote mawili ya Simba akifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya bao la pili kwa John Bocco katika mchezo wa leo dhidi ya Namungo Fc ambao wamechakazwa uwanjani kwa mabao 2-1 na kikosi hicho cha msimbazi.

Taji hili linakuwa la pili kwa Luis akiwa ndani ya  Simba baada ya kuanza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na leo kupokea taji la Shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala