Connect with us

Makala

Longstaff Kupigiwa Hesabu Ac Milan

Mkataba wa kiungo wa Newcastle United ,Matty Longstaff unameguka Juni 30 msimu huu, huku Klabu ya Ac Milan ikiwa kwenye mstari wa mbele  kuisaka saini yake.

Longstaff  yupo tayari kuongeza kandarasi nyingine iwapo klabu hiyo itakamilisha dili la kupata mmiliki mpya wa klabu hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 20 imeelezwa kuwa yupo tayari kufanya kazi na bosi mpya anayetajwa  kuwa mmoja ya wamiliki wa klabu hiyo ambayo ni kampuni kutoka Uarabuni.

Msimu huu Longstaff  amecheza mechi 13 ambapo alianza kwenye mechi 11 amefunga mabao matatu kwenye jumla ya mashindano yote.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala