Connect with us

Makala

Lomalisa Arejea Yanga sc

Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga sc Joyce Lomalisa Mutambali ameanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake wa klabu ya Yanga sc kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrekh utakaofanyika hapa nchini siku ya Jumamosi Septemba 30.

Awali beki huyo aliumia katika mchezo dhidi ya Namungo Fc na kulazimika kutolewa nje kwa matibabu zaidi lakini kwa mujibu wa Daktari wa klabu hiyo Moses Etutu kuwa mchezajji huyo tayari yuko sawa na ameanza mazoezi na wenzake.

“Ni kweli Lomalisa aliumia katika mchezo dhidi ya Namungo Fc lakini baada ya kumfanyia vipimo tuligundua kuwa damu imevilia katika misuli hivyo baada ya kumtibia kwa muda wa wiki moja sasa tayari amepona na ameanza mazoezi na wenzake.

“Kwa kawaida sio jeraha kubwa wala dogo lakini kutokana na vifaa tulivyonavyo ndio maana amerudi mapema zaidi na bahati nzuri ameweza kurecover mapema tunashukuru”Alimalizia kusema daktari huyo.

Yanga sc inakabiriwa na mchezo mgumu dhidi ya Al Merrekh siku ya Jumamosi ambapo sare ama ushindi wowote utawapeleka katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa hasa baada ya kuwa na mtaji wa mabao 2-0 waliyoshinda ugenini nchini Rwanda wiki chache zilizopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala