Connect with us

Makala

Lamine Wa Yanga Hadi 2023

Yanga Sc kupitia kwa mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM,Hersi Said wamethibitisha kumuongezea mkataba beki wao wa kimataifa,Lamine Moro ambaye iliripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufikia ukingoni msimu ujao 2021.

Lamine alijiunga na wanajangwani hao kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcon ya Zambia na kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja mabosi hao wameamua kumpa dili jipya hivyo atabakia Yanga hadi mwaka 2023.

Ndani ya ligi kuu bara amecheza mechi tatu msimu wa 2020/21 amefunga mabao mawili akiwa ni kinara wa kutupia mabao ndani ya Yanga iliyofunga mabao manne ikiwa imecheza mechi nne.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala