Connect with us

Makala

Kumradhi!

Klabu ya Simba sc imeomba radhi kwa mashabiki,serikali na wapenzi wa soka nchini hasa wenye imani ya Kikristo kutokana na kuonekana kwa maudhui yasiyofaa katika siku ya tamasha la Simba day ambalo lilifanyika siku ya Jumatatu August 8 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika tamasha hilo ambapo kulikua na matukio mengi mazuri lakini moja ya tukio lililozua taharuki ni lile la msanii Tundaman kuingia jukwaani akiwa na Jeneza pamoja na msanii mwenzie Stan Bakora kuingia na mavazi ya kikasisi na kichungaji hali iliyotafsiriwa kama dhihaka kwa waamini wenye imani ya dini ya Kikristo nchini.

Kufuatia suala hilo kuzua mjadala hadi baadhi ya viongozi wa dini kutoa maoni yao yaliyoonyesha kutofurahishwa na jambo hilo,Klabu hiyo imeamua kuomba radhi kwa wote waliokwazika kupitia barua iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala