Connect with us

Makala

Kiungo wa Mwigulu Atua Kmc

Kiungo Kenny Ally amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Kmc inayomilikiwa na Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya Singida United.

Kiungo huyo aliyepata umaarufu akiwa na Mbeya city amejiunga na Kmc japo hapo awali iliripotiwa kuwa atajiunga na Yanga kwa msaada wa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye atagharamia usajili wake kama mchango wake  klabu hiyo ambayo yeye ni mshabiki wa kutupwa.

Taarifa zinasema Kenny aliwasiliana na Singida united kabla ili kujua hatma yake na pia malipo ya mishahara inayofikia takribani milioni 14 lakini aliruhusiwa kujiunga na klabu nyingine na ndipo alisikiliza ofa ya Kmc huku Yanga ikiwa kimya bila taarifa zozote.

Hata hivyo inasemekana tayari Mheshimiwa Mwigulu ameshatimiza ahadi yake ya kusajili mchezaji mmoja kwa kufanikisha usajili wa Ally Mtoni Sonso kutoka Lipuli Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala