Connect with us

Makala

Kisinda Akwama Yanga sc

Winga Tuisila Kisinda amekwama kuitumikia klabu ya Yanga sc mpaka dirisha dogo la mwezi januari baada ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kukataa kuidhinisha usajili wake katika mfumo wa usajili nchini kupitia shirikisho la soka nchini Tanzania (Tff).

Awali Yanga sc ilikamilisha usajili wa mkopo wa kiungo huyo wa pembeni mwenye kasi na kumtoa Lazarus Kambole ambaye amekumbwa na majeraha ambayo yatamchukua muda mrefu kuwa fiti kuitumikia klabu hiyo hivyo usajili wa Kisinda ulikua na lengo la kuziba nafasi hiyo lakini kamati hiyo yenye maamuzi ya mwisho imekataa usajili huo kwa maana Yanga sc itakua na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12.

Yanga sc sasa watalazimika kusubiri mpaka dirisha dogo ili kufanya mabadiliko hayo ya usajili baada ya kumalizana na Rs Berkane juu ya usajili wa mkopo wa Kisinda ambaye kocha mpya wa Berkane amekataa kumpa nafasi kikosini humo na kumruhusu kuondoka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala