Connect with us

Makala

Kipa Mbrazil Atua Simba sc

Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa golikipa Jefferson Luis kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Resende FC kutoka Brazil ambapo msimu uliopita ameichezea Itabirito FC-MG kwa mkopo.

Kipa huyo amesajili kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho ambacho kitamkosa kipa Aishi Manula ambaye ni majeruhi wa muda mrefu na anatarajiwa kurejea mwanzoni mwa mwezi wa kumi kutokana na kuwa na majeraha ya mguu.

Kipa huyo tayari amesharipoti katika kambi ya timu hiyo nchini Uturuki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambapo pia kikosi hicho kitashiriki michuano maalumu ya Super League.

Jefferson ana uwezo mkubwa wa kulinda lango huku akitumia miguu yote kwa ufasaha pamoja na kumudu kuanzisha mashambulizi huku akiwa ana urefu wa futi 1.92 anakuja kuungana na walinda milango, Aishi Manula, Ally Salim na Ahmed Feruzi ‘Teru’.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala