Connect with us

Makala

Kinda Azam Fc Aitwa Stars

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Morocco amemuongeza kinda wa klabu ya Azam Fc Adolph Mtasingwa Bitegeko katika kikosi cha timu hiyo iliyoko kambini ikijiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la dunia 2026 dhidi ya Zambia na Algeria.

Kinda huyo amejumuishwa kwenye kikosi hicho ili kuboresha eneo la kiungo baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha timu ya Azam Fc akiisaidia klabu yake kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu ya Nbc nchini huku pia ikifika fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb.

Bitegeko amekua akipangwa mara kwa mara na mwalimu Yousouph Dabo sambamba na Yahaya Zayd katika eneo la kiungo cha chini kiasi cha kuziba vyema pengo la Sospeter Bajana ambaye ni majeruhi.

Kinda huyo pia anafaidika na nidhamu yake ya kukaba na kutekeleza kile alichotumwa na mwalimu kwa ufanisi wa hali ya juu akiwa pia na uzoefu wa kucheza mechi kubwa dhidi ya Simba sc na Yanga sc ambako amekua akikabiliana na mastaa kama Stephan Aziz Ki na Cletous Chama.

Azam Fc ili msajili mchezaji huyo dirisha dogo la Januari mwaka huu akitokea timu ya Volsungur IF ya nchini Iceland baada ya mkataba wake kumalizika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala