Connect with us

Makala

Kilimanjaro Queens Waipa Kichapo Uganda Cha Mabao 2-1

Timu ya taifa ya wanawake Kilimanjaro Queens wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada ya kuipa kichapo  Uganda kwenye mchezo wa kufuzu tiketi ya kushiriki kombe la dunia uliochezwa leo katika uwanja wa taifa jijini Dar-es-saalam.

Uganda ilianza kupata bao la kwanza kupitia Nalukende Julieth dakika ya 47 na bao la kusawazisha kwa timu ya Tanzania lilifungwa dakika ya 58 kupitia Diana Lucas.

Opah Clement aliongeza bao la pili kwa timu ya Tanzania dakika ya 68 kutokana na uzembe wa mabeki wa Uganda kupitia kona aliyopiga Diana Lucas.

Mechi ya marudio ya kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia itakayofanyika nchini India Julai 2-22 inatarajiwa kufanyika nchini Uganda tarehe 1Februari,2020.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala