Connect with us

Makala

Kilimanjaro Queens “Tunataka Kombe”.

Timu ya wanawake nchini Tanzania Kilimanjaro Queens imewafunga Burundi mabao 5-1 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki kombe la dunia kwa wanawake.

Kocha mkuu wa timu hiyo Bakari Shime ndiye aliyeongoza kikosi chake cha Kilimanjaro Queens U 17 kupata ushindi dhida ya Burundi siku ya jana katika uwanja wa Taifa nchini Tanzania.

Queen Aisha Masaka alifunga mabao mawili  dakika ya 7,10 baada ya kumchenga Amissa Inarukindo mlinda mlango wa burundi  huku Joyce Meshack alifunga bao la tatu dakika ya 33 na Protasia Mbunda bao la nne dakika ya 45.

Aisha Masaka alifunga tena bao la tano dakika ya 56 na bao la kufuta chozi kwa timu ya wanawake Burundi lilifungwa na Nadine Ndayishimiye dakika ya 69.

Mchezo huo unatarajiwa kurudiwa Januari 25 nchini Burundi na mwishoni mwa mwaka katika kuwania kombe la dunia nchini India.

Nahodha wa Burundi Peace Olga amesema kilichowaponza ni uwanja mkubwa na nyasi ni tofauti na kwao walivyozoea nyasi za bandia na uwanja wa saizi ya kati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala