Connect with us

Makala

Kichuya Yupo Bongo,Anasikilizia Mchongo Tu

Winga wa zamani wa Simba sc Shiza Ramadhani Kichuya yupo nchini Tanzania akitafuta timu ya kuchezea baada ya ile ya Awali ya NPPI ya nchini Misri kumaliza mkataba nayo ambao ulikua wa miezi sita.

 

Winga huyo aliyesajiliwa na Simba sc akitokea Mtibwa amesema kuwa kwa sasa yupo nchi huku wasimamizi wake wakimtafutia timu nje ya nchi japo tayari kuna ofa kadhaa ambazo bado wanazijadili huku wakitafuta ofa nzuri zaidi hasa barani ulaya.

Mchezaji huyo amesisitiza hatamani kucheza ligi ya Tanzania maana ni kama atakua amerudi nyuma japo hana budi kufanya hivyo endapo hatapata timu nje ya nchi.

“ Unaporudi nyuma unatakiwa kufanya kazi kubwa kurudi pale ulipokuwa mwanzo lakini kama itashindikana inawezekana ukarudi na kujipanga ili kurudi ulipokuwa au zaidi ya ulipokuwa lakini lengo kubwa ni kupata changamoto nje ya Misri na Tanzania”.

Kichuya alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro na baada ya kudumu klabuni hapo kwa takribani miaka miwili na nusu alijiunga na klabu hiyo ya NPPI ya nchini Misri kwa mkataba mfupi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala