Connect with us

Makala

Kayoko Akabidhiwa Derby

Mwamuzi wa Kimataifa wa Tanzania ,Ramadhan Kayoko Ndiye atakayechezesha Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba ambayo inatarajia kufanyika Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 23.

Kayoko amekua na uzoefu wa kuchezesha michezo hiyo akiwa ameshazesha mara kadhaa pasi kuzua malalamiko makubwa tofauti na wenzake mabao mara kadhaa wameshindwa kuhimili presha ya mchezo huo.

Refa huyo atasaidiwa na Ramadhani Mkono kutoka Tanga na Janeth Balama kutoka Iringa huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Sasii kutoka Dar es salaam ambapo waamuzi hao kwa pamoja ndio watakaoamua hatma ya wababe hao wa ligi kuu nchini nani akae kileleni baada ya dakika tisini za mchezo huo ambao Yanga sc ndio watakua wenyeji.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala