Connect with us

Makala

Kada Atua Azam Fc

Azam FC imemalizana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Tanzania Praisons, Ismail Aziz Kada siku ya leo baada ya kufuzu vipimo vya afya huku akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Ndani ya Tanzania Prisons Kada amehusika kwenye jumla ya mabao 10 kati ya 35 yaliyofungwa ndani ya timu hiyo huku akitupia jumla ya mabao matano na kutoa asisti tano za mabao kwa wachezaji wenzake.

Usajili huu unakuwa wa nne kwa Azam FC, baada ya usajili kufunguliwa Agosti Mosi ambao ulianza na Awesu Awesu, Ally Niyonzima na Ayoub Lyanga wakiwa wote wamesaini kandarasi ya miaka miwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala