Connect with us

Makala

Jezi Yanga sc Bab Kubwa

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuzindua jezi zake toleo maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambapo klabu hiyo inashiriki katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Jezi hizo za aina tatu zilizozinduliwa ni za nyumbani,ugenini na jezi ya akiba huku jezi ya nyumbani ikibadilishwa rangi na kuwa nyeusi na ugenini itatumika ya njano na kijani itakua jezi ya kati ya akiba ambapo itatumika pale kutakapokua na mwingiliano wa rangi za jezi za nyumbani na ugenini.

Katika uzinduzi huo wa jezi ambazo zimebuniwa na nguli wa fasheni nchini Sharia Ngowi ambapo alisema kuwa amechukua mawazo tofauti tofauti kutengeneza jezi hizo kulingana na tamaduni za klabu ya Yanga sc.

Jezi hizo tayari zinapatikana madukani kwa bei elekezi ya shilingi elfu hamsini ambapo pia zitakua na mdhamini mpya kifuani ambapo kampuni ya vifaa vya majumbani ya Hier ndio watakua wadhamini wakuu watakaokaa kifuani badala ya mdhamini mkuu wa siku zote kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa ambao kanuni za Caf haziwaruhusu kukaa kifuani.

Yanga sc imepata dili hilo nono la udhamini kwa mamilioni hayo ya fedha kwa muda wa michezo ya makundi tu ya kombe la shirikisho ambapo endapo wakitolewa basi wataendelea kuvaa jezi za Sportspesa katika ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala