Connect with us

Makala

Jembe La Yanga Atua Azam

Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji kutoka Rwanda ambaye alikuwa akicheza ndani ya Yanga Sc, Ally Niyonzima kwa mkataba wa miaka miwili.

Niyonzima aliyekuwa akicheza Rayon Sports Ya Rwanda pia yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao huku usajili wa kwanza ni wa kiungo Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar.

Usajili wake wa leo Agosti Mosi ni sehemu yamapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba,pia amesini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala