Connect with us

Makala

It’s Real Madrid Again

Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la klabu bingwa barani ulaya ikimfunga Liverpool Fc 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Stadium de France uliopo St.Dennis jijini Paris Ufaransa.

Licha ya Liverpool kushambulia kwa kasi kwa dakika zote 90 za mchezo lakini Uimara wa kipa Thibaus Courtois kuwa imara na kuokoa michomo mingi iliyopigwa na Mo salah na wenzake Luis Diaz na Sadio Mane.

Vinicius Jr alipokea pasi ya upendo kutoka kwa Vervede na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Liverpool na kujaa wavuni dakika ya 59 ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka mwisho mwa mchezo huo na kuipa Real Madrid taji la 14 la ubingwa wa ulaya huku ndoto za Liverpool kutwaa mataji matatu msimu huu ikiyeyuka kama maji.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala