Connect with us

Makala

Ihefu Yailaza Yanga sc

Ihefu Fc imefanikiwa kuchukua alama tatu kutoka kwa Yanga sc baada ya kufanikiwa kuifunga klabu hiyo kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Highland Estates ulioko eneo la Ubaruku mjini Mbarari mkoani Mbeya.

Ikianza na mastaa wachache wanaokaa benchi akiwemo Zawadi Mauya,Salum Abubakar na Kibwana Shomari ilianza kupata bao mapema dakika ya tatu ya mchezo kupitia Pacome Zouzou akiunganisha pasi ya Clement Mzize aliyemzidi maarifa Juma Nyoso.

Bao hilo lilisawazishwa na beki Lenny Kisu dakika ya 40 baada ya makosa ya kipa Djigui Diarra ambaye alishindwa kuucheza vyema mpira uliopigwa na Never Tigere na kuupangua vibaya ambapo ulimkuta mfungaji akiwa bila kukabwa na kufunga kwa kichwa.

Kipindi cha pili kilikua cha Charles Ilanfya aliyeunganisha kwa shuti kali pasi kutoka upande wa kulia mwa uwanja ambapo pamoja na juhudi za Yanga sc kutafuta goli la kusawazishwa lakini ilikua ngumu mpaka dakika tisini za mchezo zilipotamatika.

Sasa Ihefu Fc imefikisha alama sita ikisogea hadi nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu nchini huku Yanga sc ikisalia katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama tisa baada ya kucheza michezo minne ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala