Kocha wa klabu ya Yanga sc amesema kuwa mchezaji wake Benard Morrison hayuko fiti kucheza zaidi ya dakika anzompa kutokana na tabia ya mchezaji huyo kutopenda mazoezi magumu hali inayosababisha akose pumzi ya kucheza dakika nyingi uwanjani.
Kocha Nabi anayesifika kwa misimamo mikali hasa kuhusu nidhamu amesema kuwa Morrison anampa dakika chache kutokana na kukosa pumzi ya kutosha huku akisisitiza kuwa hapangi kikosi kutokana na kelele za mashabiki bali anaangalia nani ana mchango mkubwa klabuni hapo.
“Watu wengi wanataka kumuona Morrison anacheza lakini sisi makocha ndio tunajua ubora wa kila mchezaji kwa kila dakika kuanzia mazoezini mpaka uwanja wa mchezo,”amesema Nabi mwenye uraia pacha wa Tunisia na Ubeligiji.
“Morrison wa Sasa ni vigumu kumpa muda zaidi ya huu tunaompa labda abadalike kwa kujiweka tayari zaidi, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana ndio maana tulimleta hapa lakini kwasasa hayuko tayari kucheza kwa muda mrefu zaidi ya huu tunaompa watu waelewe hili”.
“Hakuna kocha ambaye ataamua kumweka nje Morrison kwa kipaji chake kama yuko sawasawa, watu wasidhani sisi makocha hatupendi kuona timu inashinda Mimi sio kocha wa kumpa nafasi mchezaji kwa jina lake au presha ya nje ya uwanja tofauti na kile anachonionyesha uwanja wa mazoezi.Alisema kocha huyo mkali lakini ana busara anapozungumza
Morrison alijiunga na Yanga sc akitokea Simba sc kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini amekua hapai nafasi ya kutosha kikosini humo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu na majeraha ya mara kwa mara.