Connect with us

Makala

Hapatoshi Fainali Ngao ya Jamii

Hapatoshi katika uwanja wa Mkwakwani ambapo Jumapili utapgwa mchezo wa fainali ya ngao ya jamii baina ya Simba sc na Yanga sc baada ya Simba sc kufanikiwa kuifunga Singida Fountain Gate kwa mabao 4-2 kwa penati.

Yanga sc ilitangulia kuingia fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Fc na sasa Simba sc imefuata huko na kusababisha michuano hiyo kugeuka kivutio kutokana na mechi hiyo kuwakutanisha mahasimu wawili wa soka nchini.

Ingawa bado makocha wa timu hizo hawajapata vikosi vya kwanza kwa asilimia mia moja lakini kurejea kwa Cletous Chama na Jesus Moloko kunawapa nafuu walimu wote hasa katika machaguo upande wa kiungo mshambuliaji.

Yanga sc mpaka sasa bado pengo la Fiston Mayele lipo wazi hasa katika mchezo dhidi ya Azam Fc ambapo mshambuliaji Kennedy Musonda ndie alikua kiongozi na alikosa utulivu na kushindwa kuhimili mikikimikiki ya mabeki wa Azam Fc mpaka alipoingia Clement Mzize.

Simba sc wenyewe bado hawana maelewano mazuri katika eneo la kiungo ambapo kocha huwategemea zaidi Mzamiru Yassin,Sadio Kanoute na Chama ama Saido kama viungo washambuliaji ambapo katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate walishindwa kufua dafu na kulazimika mwalimu kumuingiza Fabrice Ngoma.

Mchezo huo utaamuliwa zaidi na mbinu za walimu Miguel Gamondi na Roberto Oliveira huku pia juhudu binafsi za wachezaji hasa matumizi ya nafasi ndio vitu ambavyo vitaamua matokeo ikizingatiwa kwamba uwanja sio mkubwa sana huku eneo la kuchezea likiwa halina ubora mkubwa sana hasa kuweza kupiga pasi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala