Connect with us

Makala

Hafiz Afunguka Kufunga Bao la Kwanza

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Hafiz Konkoni amefunguka kufunga bao la kwanza akiwa na timu yake mpya ya Yanga sc mara baada ya kusajiliwa na timu hiyo kuziba nafasi ya Fiston Mayele ambaye amejiunga na Pyramids Fc ya nchini Misri.

Hafiz ambaye katika mchezo huo wa kwanza wa ligi kuu kwa timu yake aliingia dakika ya 69 akichukua nafasi ya Kennedy Musonda na kufanikiwa kufunga bao la tatu akimalizia mpira uliokua unazagaa ambapo timu yake ilifunga jumla ya mabao 5-0 katika mchezo huo.

“ Kufunga bao la kwanza katika mazingira kama haya sio rahisi. Nilipokuja kwenye timu hii ya Young Africans walikuwa na mmoja wa washambuliaji bora barani Afrika, Fiston Mayele, ni presha kubwa kuziba pengo lake. Nilihitaji bao hili ili kupunguza presha, Nawaahidi kazi nzuri, ”Alisema

Yanga sc ina kibarua kigumu cha kutetea makombe yake matatu msimu huu ambapo tayari wamelikosa kombe la ngao ya jamii ambalo limechukuliwa na Simba sc na sasa inawapasa kupambana kuchukua makombe ya ligi kuu na ngao ya jamii.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala