Connect with us

Makala

Greenwood Ashutumiwa kwa Ubakaji

Kinda wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood 20 amekamatwa na polisi wa jiji la Manchester kufuatia kusambaa wa video ikimuonyesha msichana mmoja akilalamika kujeruhiwa na staa huyo wakati akilmazimisha kufanya ngono.

Msichana huyo anayefahamika Harriet Robson inasemekana alikua ni mpenzi wake wa siku nyingi lakini staa huyo alitumia nguvu kumlazimisha kufanya mapenzi kinyume na matakwa yake hivyo kumjeruhi sehemu mbalimbali ikiwemo mdomoni na mikononi.

Kufuatia tukio hilo tayari klabu yake ya Manchester United imemkataza kuhudhuria mazoezi ama mechi huku ikisitisha kuuza bidhaa za mchezaji huyo ambapo pia baadhi ya mastaa wa klabu hiyo kama Cristiano Ronaldo,Paul Pogba,Edson Cavani,Phill  Jones na David De Gea wameamua kusitisha urafiki na staa huyo katika mitandao ya kijamii hasa instagram.

Pia suala hilo licha ya kuwa na madhara zaidi katika soka la kinda huyo ambaye alisaini mkataba wa miaka minne kusalia Man united mwaka 2019 pia limeharibu mahusiano ya kibiashara na wadhamini wake kampuni ya Nike ambao nao wamemuondoa katika orodha ya mastaa  wanaowadhamini.

Staa huyo endapo atakutwa na hatia ana hatihati ya kufungwa miaka 30 jela huku pia ikionekana kuwa nidhamu ni tatizo kwake ambapo mwaka 2019 alifukuzwa kambini na kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate kwa kuvunja sheria za kukaa karantini kipindi cha ugonjwa wa Corona nchini Iceland.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala