Connect with us

Makala

Goti lampeleka Yacouba Tunisia.

Klabu ya soka ya Yanga imethibitisha kumpeleka nchini Tunisia straika wake Yacouba Songne kutokana na marehana ya goti aliyoyapata katika mchezo wa NBC premier league dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo ulifanyika kwenye dimba la Benjamini Mkapa Yacouba alitolewa mapema kipindi cha pili baada ya kuumia goti.

Licha ya kutolewa katika mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Saido Ntibanzokiza Yanga ilifanikiwa kushinda mchezo huo kwa ushindi wa 3-1 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 15 baada ya michezo mitano.

Taarifa hiyo ya safari yake imethibitishwa kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu ya Yanga mapema hii leo.

Huenda mshambuliaji huyo akakosa hadi mwakani kutokana na historia ya majeraha ya goti kuwaweka nje kwa muda mrefu wachezaji mbalimbali,Yacouba yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na kocha mkuu wa timu hiyo Nasreedin Nabi anamhitaji mchezaji aongezewe mkataba kwani yupo kwenye mipango yake.

Kuumia kwa mchezaji huyo huenda ikawa habari njema kwa wachezaji wa Kitanzania Farid Musa na Dickson Ambundo wanaocheza nafasi yake kumuonesha mwalim Nabi kuwa wanastahili kucheza kikosi cha kwanza.

Lakini pia italipa nafuu benchi la ufundi katika machaguzi ya wachezaji nane wanaotakiwa kuhusika katika mchezo mmoja wa ligi kikanuni kwani tayari Yacouba hayupo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala