Connect with us

Makala

Geita Gold Yaihamishia Yanga sc Kirumba

Timu ya Geita Gold Sc imehamisha mchezo wake wa ligi kuu ya soka ya Nbc dhidi ya Yanga sc katika uwanja wa Ccm Kirumba uliopo jijini Mwanza badala ya uwanja wake wa kila siku wa shule ya wasichana ya Nyakumbu iliyopo mkoani humo.

Mabadiliko hayo ya uwanja ni kwa mujibu wa kanuni ya ligi kuu kuhusu uwanja 9:7 ambapo timu ya ligi kuu inaruhusiwa kuchagua uwanja inayotaka katika michezo miwili ya nyumbani na kuwasilisha maombi hayo kabla ya siku 21.

Inatajwa sababu kubwa ya kuhamisha mchezo huo ni kutokana na kuongeza mapato zaidi ambapo uwanja wa Ccm Kirumba una uwezo wa kuingiza mashabiki wengi zaidi kuliko ule wa Nyankumbu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala