Connect with us

Makala

Geita Gold Hoi kwa Maafande wa Ruvu

Klabu ya Ruvu shooting imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani jioni ya leo.

Mabao ya Ruvu Shooting yamefungwa na Hamad Majimengi dakika ya 53 na Elias Maguri dakika ya 87 baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Offen Chikola dakika ya 24 ambaye aliwapiga chenga wachezaji takribani watatu wa Ruvu shooting.

Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 31 za mechi 23 sasa nafasi ya tano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala