Hatimaye makocha wa klabu za Simba sc Fadlu Davis na wa Yanga sc Miguel Gamondi wameanza tambo kuelekea mchezo huo utakaofanyika Oktoba 19 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Gamondi kwa upande wake amesisitiza kuhitaji alama tatu muhimu katika mchezo huo licha ya kukiri kuwa mpinzani wake yupo vizuri.
“Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa na historia ya mafanikio. Tunawaheshimu sana kama wapinzani, lakini tunajipanga vizuri kwa mchezo huu”.
“Tunafahamu wanavyocheza na nguvu yao, lakini tutatumia maandalizi yetu kuleta ushindani na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kutumia nafasi kufunga mabao”.Alisema Gamondi ambaye hutumia namba kumi watatu eneo la ushambuliaji
”Simba Sc wana ndoto ya kutufunga ili wafurahi sisi tunataka kuwafunga ili tuwe mabingwa hiyo ndio tofauti”.Aliendelea kusema Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga sc raia wa Argentina.
Nae kwa upande wake Fadlu Davis kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc yeye ameendelea kusema kuwa anaamini nidhamu ndio jambo muhimu zaidi ili kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Tunajua ubora wa Yanga, lakini tunajiandaa kimkakati. Lazima tuwe makini kwa kila dakika, kujenga mashambulizi kwa kasi na kudhibiti safu ya ulinzi kwa umakini mkubwa”.Alisema Fadlu raia wa Afrika ya kusini.
Fadlu anaamini kutumia fursa chache zinazopatikana ni muhimu, akiongeza kwa kusema kuhusu kutumia nafasi hizo.
“Katika mechi kama hizi, nafasi ni chache, hivyo tunahitaji kuwa bora katika kutumia na kumalizia nafasi hizo”.
Simba sc na Yanga sc zinatarajiwa kukutana Oktoba 19 2024 ambapo Simba sc imepoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya Yanga sc.