Connect with us

Makala

Gamondi Awaita Mashabiki

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi amewaita mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu wa klabu hiyo dhidi ya Kmc utakaofanyika Augusti 23 katika uwanja wa Chamazi Complex ulioko Mbagala Chamazi.

Yanga sc inautumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa katika matengenezo makubwa.

Katika mchezo huo Yanga sc itahitaji ushindi kwa hali na mali ikizingatiwa kuwa mtani wake Simba sc tayari yupo kileleni mwa msimamo akiwa na alama sita huku Kmc wenyewe wakiwa tayari na alama moja baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu kwa timu hizo.

Akizungumzia hali ya kikosi chake kocha Gamond alisema kuwa vijana wake wapo vizuri kupambana kupata alama tatu hivyo wanawaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuongeza morali kwa wachezaji wake.

“Ratiba ni kweli ni ngumu kutokana na ratiba ya michezo kuwa mingi lakini hiyo ndio kazi yetu. Tunapaswa kujiandaa kama timu kubwa ili kupata matokeo chanya katika kila mechi,ni mchezo wetu wa kwanza wa ligi na matarajio yetu ni kushinda,kwa timu kama Yanga kila mechi matarajio yetu ni ushindi,”

“Nawasihi mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kesho, Tutacheza kandanda safi na la kuvutia ili tupate matokeo, Tupo kwenye njia sahihi, tumejipanga na tumejiandaa kuwapa burudani”Alisema Gamondi

Tangu atue Yanga sc kocha huyo amefanikiwa kutengeneza kikosi imara sana hasa eneo la ulinzi na kiungo huku akipata shida katika eneo la ufungaji kutokana na safu hiyo kukosa mabao ya mara kwa mara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala