Connect with us

Makala

Fifa Yawashukia Tabora United

Klabu ya Kitayosce ambayo zamani Tabora United imefungiwa kusajili Kutokana na kushindwa kumlipa fedha za usajili na baadhi ya mishahara aliyekuwa Mlinzi wao wa kushoto raia wa Ghana Asante Kwasi.

Baada ya mgogoro huo Asante kwasi alikimbilia shirikisho la soka duniani (FIFA) ambapo alishinda shauri hilo na klabu ya hiyo kuamliwa kumlipa stahiki zake ndani ya siku 45 kitu ambacho hakikufanyika mpaka hapo ilivyoamliwa na shirikisho hilo kumlipa.

Tabora United sasa wamefungiwa kusajili wachezaji wa kimataifa na wale wa ndani mpaka hapo watakapolipa fedha hizo ambapo watafunguliwa kusajili moja kwa moja.

Timu hiyo imekua na matatizo kadhaa hasa katika masuala ya usajili kutokana na ugeni wake katika ligi kuu baada ya kupanda daraja ambapo katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ilicheza ikiwa na wachezaji nane pekee na hivyo mchezo ulivunjika baada ya baadhi ya wachezaji kupata majeraha/

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala