Connect with us

Makala

Fei,Zimbwe Watemwa Stars

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambacho kitaingia katika mchezo wa kufuzu fainali ya mataifa ya Africa (Afcon) dhidi ya Algeria tayari kimeingia kambini nchini Tunisia kujiandaa na mchezo huo.

Katika kikosi hicho ambacho tayari kimesafiri majina makubwa baadhi yamekosekana tofauti na matarjio ya wengi huku wachezaji kama Jonas Mkude na John Boko wakishangaza wadau kutokana na kuitwa kwao huku katika klabu zao wakiwa wanakaa benchi.

Katika kikosi hicho mastaa kama Feisal Salum,Salum Abukabari,Mohamed Hussein na Shomari Kapombe wameachwa huku nafasi zao zikizibwa na Mudathiri Yahaya,Abdi Banda,Dickson Job na wengineo.

Mwalimu Adel Amrouche ameonekana kupendelea zaidi wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuzuia ili kupata alama moja ambayo itaisaidia Stars kufuzu kwa mara ya tatu katika historia ya michuano hiyo.

Kikosi kamili kilichoitwa ni kama kifuatacho:

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala